Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:57

Jenerali Karake wa Rwanda aachiwa huru

Waziri wa sheria wa Rwanda Busigye Johnstone akizungumza na waandishi wa habari na wafuasi wa Kareke mjini london.
Waziri wa sheria wa Rwanda Busigye Johnstone akizungumza na waandishi wa habari na wafuasi wa Kareke mjini london.

Uamuzi huo wa Jumatatu una maana kwamba generali Karenzi Karake ambae ni kiongozi muhimu katika serikali ya rais Paul Kagame, anaweza kurudi nyumbani.

Mahakama moja ya uingereza imetupilia mbali kesi yenye utata dhidi ya kiongozi wa ujasusi wa Rwanda anayehitajika Spain kwa uhalifu wa makossa ya jinai.

Uamuzi huo wa Jumatatu una maana kwamba generali Karenzi Karake ambae ni kiongozi muhimu katika serikali ya rais Paul Kagame, anaweza kurudi nyumbani.

Mahakama hiyo mjini London imesema kuwa sheria za Uingereza haziruhusu kusikilizwa kesi dhidi ya tuhuma zilizofanyiwa nje ya nchi na mtu asie na asili ya Uingereza.

Wafuasi wa Karage wakiandamana mjini London kupinga kukamatwa kwake.
Wafuasi wa Karage wakiandamana mjini London kupinga kukamatwa kwake.

Uingereza ilimkamata Karake mwezi Juni ikifuata amri ya kukamatwa kutoka Uhispania kwa madai kuwa generali huyo alihusika kwenye uhalifu wa jinai baada ya mauaji ya halaiki ya 1994 huko Rwanda.

Alikuwa mmoja wa viongozi 40 wa ngazi za juu waliotuhumiwa na Spain kwa mauaji ya kundi la maafisa wa afya wa wahispania wakujitolea waliouwawa katika miaka ya 90.

Kukamatwa kwa Karange kulizuhs amajibu yenye hasira kutoka serikali ya Rwanda iliyodai kuwa zoezi hilo lilikuwa na ushawishi wa kisiasa.

Wakati huo huo mwezi uliopita maandamano makubwa yaligubika ubalozi wa uingereza nchini Rwnda ili kutoa shinikizo la kuachiliwa kwa jenerali huyo.

XS
SM
MD
LG