Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:59

Jaribio la mapinduzi limefeli Sao Tome, kiongozi ameuawa


Watu wanne wameuawa katika jaribio la mapinduzi ambalo limefeli nchini Sao Tome.

Mkuu wa jeshi amesema kwamba amethibitisha idadi hiyo ya watu waliouawa.

Jeshi lilizima jaribio hilo la mapinduzi katika nchi hiyo ndogo inayozungumza kireno iliyo karibu na Afrika ya kati, na ambayo inachukuliwa kama yenye ukomavu wa demokrasia.

Makabiliano ya risasi yametokea katika kambi ya jeshi.

Waziri mkuu Patrice Trovoada, ameambia shirika la habari la STP kwamba raia wanne na wanajeshi, pamoja na wapiganaji kutoka kundi la Afrika kusini lililopigwa marufuku la Buffalo wamehusika katika jaribio hilo la mapinduzi saa za usiku.

Wanajeshi 12 wamehusika katika jaribio hilo na wamekamatwa wakijaribu kuvamia kambi za jeshi.

Kati ya waliouawa ni Arlecio Costa ambaye alikuwa mpiganaji katika kundi la mamluki la Afrika kusini la Buffalo, lililopigwa marufuku mnamo mwaka 1993. Jeshi limesema kwamba ndiye alikuwa anaongoza jaribio hilo la mapinduzi na ameuawa.

XS
SM
MD
LG