Chombo hicho aina ya H2A kimerushwa na kampuni ya Mitsubishi Heavy Industries, kutoka kwenye kituo cha anga za juu cha Tanegashima, kusini magharibi mwa Japan, kikiwa kimebeba satellite yenye uwezo wa kupiga picha, kama sehemu ya juhudi za Tokyo za kuimarisha uwezo wake wa kijeshi.
Kituo cha Satellite cha serikali pamoja na kampuni ya Mitsubishi wamesema kwamba zoezi hilo limefanyika kwa mafanikio kwa kuwa satellite hiyo aina ya Optical -8 ilitenganishwa na roketi na kuingia kwenye anga za juu kama ilivyopangwa.
Japan ilianza program ya kutengeneza satellite hiyo baada ya Korea Kaskazini kurusha silaha kwenye anga yake hapo 1998. Japan inalenga kutengeneza mtandao wa satellite 10 zikiwemo zile zinazobeba radar zenye uwezo wa kufanya operesheni nyakati za usiku, au wakati wa hali ngumu ya hewa, pamoja na uwezo kutoa onyo la mapema kuhusu urushaji wa silaha.
Forum