Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 18:52

Japan yakemea mkanda wa video wa Islamic State


Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amelitaka kundi la Islamic State liwaachie mara moja mateka wawili iliowaonyesha kwenye mkanda wa video ikitishia kuwaua.

Kundi hilo la Islamic State limeda kwamba kama Japan haitowalipa dola milioni 200 itawaua watu hao wenye asili ya Japan.

Bwana Abe, ameonyesha kuchukizwa Jumanne, saa kadhaa baada ya wanamgambo hao kutoa mkanda wa video.

Katika mkanda huo wa video unaomwonyesha mtu mmoja anayeongea kiingereza akiwa amevalia mavazi meusi na kujiziba uso akiwa ameshikilia kisu.

Aidha mtu huyo anaonekana pamoja na watu wawili waliopiga magoti wakiwa na mavazi ya rangi ya chungwa.

Wanamgambo hao wamewatambulisha watu hao kuwa ni Kenji Goto, na Haruna Yakawa, na kuikosoa Japan, kwa kusaidia juhudi za wanamgambo wa magharibi kupambana na Islamic State.

XS
SM
MD
LG