Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 06:27

Japan yapongeza ushirikiano wake na Marekani


Rais Barack Obama na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe wameweka mashada ya maua huko Arizona kwenye kumbukumbu ya Peal Harbor.
Rais Barack Obama na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe wameweka mashada ya maua huko Arizona kwenye kumbukumbu ya Peal Harbor.

Ziara hii imeongeza zingatio la ushirikiano wa hivi sasa kati ya Marekani na Japan ambazo ziliingia katika mapigano makali baina yao katika vita vya pili vya dunia.

Wiki hii, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amefanya ziara ya kihistoria kwenye Pearl Harbor katika jimbo la Marekani la Hawaii.

Abe alikwenda katika eneo hilo akiwa na mwenyeji wake Rais Barack Obama.

Viongozi hao walitanguliza umuhimu wa suala zima la suluhu. Obama amesema: “Vita vinaweza kumalizika, na pia mahasimu wakubwa wanaweza kurejea kuwa washirika na marafiki wakubwa.”

Waziri mkuu huyo alionyesha kuguswa na wale waliokufa kufuatia mashambulizi ya Japan Pearl Harbor miaka 75 iliyopita.

Alitoa “rambi rambi zake za dhati” kwa vifo vya wapiganaji wamarekani zaidi ya 2400 waliouwawa wakati wa mashambulizi hayo.

Abe aliungana na Obama katika kuweka mashada ya maua kwenye sehemu hiyo ya kumbukumbu ya Arizona. Kumbukumbu hii imejengwa ndani ya meli ya kivita iliyokuwa imeharibiwa na shambulio hilo la Disemba 7, 1941.

Ziara hii imeongeza zingatio la ushirikiano wa hivi sasa kati ya nchi hizi mbili ambazo ziliingia katika mapigano makali baina yake katika vita vya pili vya dunia.

Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe wakiwa huko Pearl Harbor.
Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe wakiwa huko Pearl Harbor.

​Katika hotuba yake huko Pearl Harbor, Abe ameuelezea uhusiano wa Japan na Marekani, “ni ushirikiano wa matumaini.” Wakati Obama ameuita ni Ushirikiano wa msingi wa eneo la Asia-Pacific na nguvu inayoleta maendeleo duniani.

Hii siyo ziara ya kwanza kufanywa katika bandari hiyo na waziri mkuu wa Japan. Lakini, ilikuwa imeonyesha wazi umuhimu wake, baada ya miaka 75 tokea tukio la kushtua la mashambulizi lililo pelekea Marekani kuingia katika vita vya II vya dunia.

Pia imekuja baada ya miezi saba tangu Obama kuwa ni Rais wa kwanza kutembelea jiji la Hiroshima nchini Japan, ambapo Marekani ilipiga bomu la atomic la kwanza lililotumika katika vita.

XS
SM
MD
LG