Vyama vya kisiasa vya upinzani katika jamhuri ya Congo vinatarajia kukutana wiki ijayo kujaidli kama vishiriki katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Machi 20.
Hii inafuatia kupitishwa hivi karibuni kwa katiba mpya ambayo imeondoa kiwango cha ukomo wa utawala na kumruhusu rais Denis Sassou Nguesso kugombea tena muhula mwingine.
Kura ya maoni ya mwezi Octoba ilipitisha kwa asilimia 92 ya kura, ikiondoa mihula miwili ya utawala na umri wa miaka 70 kwa wagombea urais.
Lakini wapinzani walidai mapendekezo hayo ni kinyume cha sheria yanayopelekea kubadili katiba. Perfect Koleas kiongozi wa upinzani wa chama cha Congolese Movement for Democracy amesema makundi yote ya upinzani yemepinga kwa nguvu harakati hizo .
Amesema hivi karibuni makundi yataamua mwelekeo wake wa baadae kuhusu upigaji kura wa mwezi Machi. Amesema upinzani hauridhishwi na uamuzi wa rais Nguesso kuondoa kiwango cha kikomo cha utawala kwa lengo la kutaka kuwania tena madaraka.