Serikali inataka wimbo huo wa kuunga mkono demokrasia uondolewe kwenye internet, na usitumiwe. Wimbo huo kwa jina Glory Hong Kong, kwa bahati mbaya uliwahi kuchezwa kwenye hafla za michezo ya kimataifa, badala ya wimbo wa taifa wa China wa March of the Volunteers.
Wakosoaji wameonya kwamba kuzuiliwa kwa wimbo huo ni mfano mwingine wa kuminywa kwa uhuru ndani ya Hong Kong, ambayo ilikuwa koloni la Uingereza. Hong Kong ilirejeshwa kwenye utawala wa China 1997, na tangu wakati huo China imekuwa ikiipokonya uhuru wake, wakati Beijing ikifanya marekebisho ya kisiasa, pamoja na kuweka sheria kali za usalama wa taifa.
Forum