Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 00:32
VOA Direct Packages

Jaji mkuu wa Iran atoa onyo kali kwa wanawake wanaokiuka maadili ya mavazi nchini humo


Picha ya maktaba ya maandamano ya Iran kufuatia kifo cha mwanamke akiwa mikononi mwa polisi.

Jaji mkuu wa Iran Gholamhossein Mohseni Ejei, amesema Jumatatu kwamba wanawake wanaokiuka madili ya kiislamu kwenye mavazi yao wataadhibiwa.

Taarifa hiyo imetolewa na chombo rasmi cha habari cha serikali cha IRNA, ikionekana kuwa himizo la sheria hiyo kali, ilyosababisha maandamano ya kitaifa kwa miezi kadhaa, na kupelekea msako mkali.

Mohseni Ejei amesema kwamba mwanamke kutovalia hijab ni sawa na kuonyesha dharau kwa taifa hilo la kiislamu pamoja na misingi yake. Amesema kwamba serikali itashirikiana na mahakama kuhakikisha kuwa wanaokiuka sheria hiyo wanaadhibiwa.

Kifo cha mwanamke wa Iran wa kikurdi Mahsa Amini Septemba 16 mwaka jana akiwa mikononi mwa polisi kwa tuhuma za kutovalia hijab, kilipelekea maandamano makubwa ya kitaifa, na kuwa changamoto kubwa zaidi kwa utawala wa kiislamu wa Iran uliyobuniwa 1979.

Msako mkali ambao umekuwa ukifanywa na maafisa wa usalama tangu wakati huo umetuliza maandamano hayo katika wiki za karibuni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG