Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 19:59

Jacob Zuma asema yuko tayari kurudi kwenye siasa licha ya tuhuma za rushwa


Rais wa zamani Afrika Kusini Jacob Zuma.
Rais wa zamani Afrika Kusini Jacob Zuma.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya rushwa na kutumikia kifungo cha muda mfupi gerezani, amesema yuko tayari kurejea katika siasa akibaki na chama tawala cha ANC

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya rushwa na kutumikia kifungo cha muda mfupi gerezani, amesema yuko tayari kurejea katika siasa akibaki na chama tawala cha ANC.

Katika taarifa yake Jumatatu usiku Zuma, mwenye umri wa miaka 80, alisema ameombwa na wanachama wa chama cha African National Congress (ANC), ambacho kimetawala Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, kujiweka mbele wakati chama hicho kikijiandaa kuchagua uongozi mpya.

“Sitakataa wito kama huo iwapo wataona ni muhimu kwangu kukitumikia tena chama hicho” alisema na kuongeza kuwa amekuwa akishauriana na viongozi wa chama licha ya ugumu unaosababishwa na hali yangu ya kisheria kwa sasa aliongeza.

Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na mvtano mkubwa ndani ya ANC, kabla ya kongamano la kitaifa la uchaguzi mwezi Desemba.

Chama kitafanya uchaguzi wa wakumchagua kiongozi mpya, ambaye hatimae atakuwa mgombea wa uchaguzi ujao wa urais mwaka wa 2024.

Rais wa hivi sasa Cyril Ramaphosa ana matumaini ya kuchaguliwa kwa mhula wa pili lakini anakabiliwa na upinzani kutoka kundi la wanachama wanaomuunga mkono Zuma, ambae ni shujaa kwa wanachama wa mashinani wa ANC licha ya kuhusika katika kashfa kubwa ya ulaji rushwa nchini humo.

Zuma anasema anamunga mkono mke wake wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma kuchukua nafasi ya Ramaphosa na amegusia kwamba yuko tayari kua mwenyekiti wa chama.

XS
SM
MD
LG