Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:50

Mfanyabiashara maarufu apigwa risasi na kuuawa Nairobi


Mr Jacob Juma
Mr Jacob Juma

Na BMJ Muriithi

Mfanyabiashara mmoja mashuhuri nchini Kenya, Jacob Juma, ambaye alijulikana kwa kuikosoa serikali kupitia mitandao ya kijamii, alipigwa risasi na watu wasiojulika na kuuawa Alhamisi usiku.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Juma, mwenye umri wa miaka 45, alipigwa risasi na watu ambao walikuwa wakiendesha pikipiki karibu na shule ya Lenana alipokuwa akielekea nyumbani kwake mtaa wa Karen mwendo wa saa nne usiku.

Taarifa zimesema gari lake aina ya Mercedes Benz lilipatikana na zaidi ya matundu 10 ya risasi.

Polisi walisema hakuna kilichoibiwa kutoka kwenye gari hilo na kwmba pesa zake na simu ya mkono Simu zilipatikana ndani ya gari.

"Tunachukulia kifo chake kama uhalifu," mkuu wa polisi mjini Nairobi aliwaambia wanahabari siku ya Ijumaa. "Tulipata Sh 6,500 na simu mbili ndani ya gari lake," aliongeza Bw Koome.

Mfanyabiashara huyo alifahamika kama mwanakandarasi aliyejihusisha katika biashara mbalimbli, pamoja na ile ya uchimbaji na uuzaji wa madini.

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga alikuwa baadhi ya watu wa kwanza kutuma risala za rambirambi kwa familia ya Bw Juma.

"Twaitaka serikali ifanye uchunguzi mara moja kufuatia kifo hicho," alisema Odinga.

Juma alikuwa mkosoaji wa serikali ya rais Uhuru Kenyatta na aliwasilisha kesi mbili mahakamani dhidi ya Naibu Rais William Ruto. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye mtandao wa Twitter siku chache kabla ya kifo chake:

Juma on twitter
Juma on twitter

XS
SM
MD
LG