Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 23:47

Kituo cha mpakani cha shambuliwa Ivory Coast


Maafisa wa kijeshi nchini Ivory Coast wanasema watu waliokuwa na silaha wameshambulia kitu cha mpakani upande wa magharibi mwa nchi katika mpaka wake na Liberia.

Maafisa wanasema mashambulizi yalifanyika karibu na mji wa Toulepleu. Wakazi mjini Toulepleu wameiambia Sauti ya Amerika kwamba watu wengi walikimbia kufuatia mapambano.

Maafisa wa Ivory Coast hawakusema kama kulikuwa na majeruhi wakati wa mapigano ya Jumatatu.

Shambulizi linafuatia jingine katika mkoa wa mpakani mwezi June ambapo walinzi saba wa amani wa Umoja wa Mataifa waliuawa.

Pia shambulizi la wiki iliyopita, ambapo watu waliokuwa na silaha waliwashambulia wanajeshi wa Ivory Coast katika mji mkuu wa kibiashara wa Abidjan na kuwaua wanajeshi 11.

Bado haiko bayana nani wanahusika na mashambulizi hayo.

Maafisa wanawalaumu wanajeshi wahuni na wanamgambo ambao bado wanamtii rais wa zamani Laurent Gbagbo.
XS
SM
MD
LG