Ivory Coast itapeleka lita milioni 50 za petroli kwa mwezi kwenda Guinea, vyombo vya habari vya serikali ya Ivory Coast vimetangaza Jumatano, kufuatia mlipuko na moto katika kituo kikuu cha mafuta nchini humo.
“Ivory Coast imeahidi kupeleka lita milioni 50 za petroli kwa mwezi kwenda Guinea,” alisema mwandishi wa habari kutoka Radio Television Ivoirienne (RTI), bila kutaja muda wa usafirishaji.
Waziri wa Fedha wa Guinea Moussa Cisse amekutana na Waziri wa Madini, Petroli na Nishati wa Ivory Coast, Mamadou Sangafowa Coulibaly mjini Abidjan Jumatano.
Mkataba utasainiwa Alhamisi, RTI iliripoti, na kuongeza kuwa Guinea inahitaji lita milioni 70 za petroli kwa mwezi. Watu 24 walifariki na wengine 454 kujeruhiwa katika mlipuko wa Desemba 18 katika mji mkuu wa Guinea, Conakry.
Forum