Baraza la mawaziri limesema kwamba hali ya afya nchini humo sasa ni nzuri na shughuli za uchumi zinaweza kuendelea kama kawaida.
Mipaka hiyo pia imefunguliwa ili kutoa fursa kwa maafisa wa usalama kukabiliana na tatizo la wahamiaji haramu.
Kila mtu anayeingia au kutoka Ivory Coast sasa anatakiwa kupitia mipaka rasmi.
Shirika la habari la ufaransa RFI limeripoti kwamba kumekuwa na ongezeko la wakimbizi wanaoingia Ivory Coast kutoka Burkina Faso, na idadi imefikia 8,700.
Wakimbizi hao wanastahili kupokelewa na kutambuliwa kwenye mipaka rasmi.