Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 14:16

Matetemeko 3 yatokea katikati ya Italy


Watalii wakipewa maelekezo katika moja ya stesheni za treni zilizofungwa baada ya tetemeko la ardhi nchini Italy.
Watalii wakipewa maelekezo katika moja ya stesheni za treni zilizofungwa baada ya tetemeko la ardhi nchini Italy.

Mfululizo wa matetemeko 3 ya ardhi yenye nguvu yametokea katikati ya Itali katika kipindi cha saa moja Jumatano.

Matetemeko hayo yametikisa katikati ya Italy katika mji ambao ulikumbwa na matetemeko makubwa mwaka jana na hivi sasa umefunikwa na theluji zaidi ya futi tatu katika siku za karibuni.

Kulikuwa hakuna ripoti za majeruhi lakini mtikisiko ulifika hadi Rome, ambako vituo vya treni vilifungwa kama tahadhari na wazazi walitakiwa kuwafuata watoto mashuleni.

Tetemeko la kwanza, la kiwango cha 5.3 kwa kipimo cha “Richter,” lilitokea upande wa magharibi wa mji wa Amatrice takriban saa 10:25 asubuhi (0925GMT), kwa mujibu wa utabiri wa idara ya Jiolojia ya Marekani.

Tetemeko la pili ambalo lilikuwa la kiwango cha 5.7 lilipiga tena eneo hilo hilo baada ya dakika 50, na dakika kumi baadae tetemeko la tatu lilitokea lenye kiwango cha 5.3. Pia kulikuwa na mitetemo ya hapa na pale katika eneo hilo.

Theluji iliyoshuka katika eneo lenye tetemeko wiki iliyopita, ambayo imejaa kwa zaidi ya mita 1.5 katika baadhi ya maeneo, imekuwa ni tatizo kwa kusafirisha mahitaji na kufikisha misaada ya dharura. Meya Maurizio Pelosi wa mji wa Capitagno, ulioko karibu kabisa na kiini cha tetemeko, amesema hata kabla ya tetemeko hilo barabara nyingi kwenda na kutoka kwenye mji huo zilikuwa hazipitiki kwa sababu ya theluji.

Mfanyakazi wa hotelini, Giuseppe Di Felice, ameiambia kituo cha radio cha RAI kinachoendeshwa na serikali kuwa watu hawakuweza kutoka nje ya nyumba zao. “Kwa kweli ni janga kubwa,” amesema.

Mji huo wenye milima ulikumbwa na matetemeko matatu mwaka jana, na kuuwa takriban watu 300 na kusababisha hasara kubwa kwa majengo ya zamani. Mnara mmoja wa kanisa la Amatrice ulivunjika Jumatano kutokana na matetemeko.

Mji huo uko umbali wa karibia kilomita 100 magharibi-mashariki mwa Rome.

Antonio Tajani, mwanasiasa wa Italy ambaye ni rais wa bunge la Ulaya, amesema matetemeko hayo yamesikika kwa umbali hadi Rome lakini inaelekea hakuna waathirika wowote kutokana na tukio hilo.

XS
SM
MD
LG