Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 02, 2024 Local time: 06:13

Italy inasema uingiliaji wa kijeshi nchini Niger utasababisha mzozo mpya wa uhamiaji


Wahamiaji waliokwama mjini Niamey, Niger, waonekana katika kambi yao ya muda, Agosti 22, 2023. Picha ya AP
Wahamiaji waliokwama mjini Niamey, Niger, waonekana katika kambi yao ya muda, Agosti 22, 2023. Picha ya AP

Waziri wa mambo ya nje wa Italy Antonio Tajani Alhamisi amesema suluhisho la kijeshi kwa mapinduzi nchini Niger itakuwa “janga” ambalo litasababisha mzozo mpya wa uhamiaji.

Jumuiya ya nchi za Afrika magharibi (ECOWAS) imekuwa ikijaribu kuzungumza na viongozi wa mapinduzi ambao walinyakua madaraka mwezi uliopita, lakini ilionya kuwa iko tayari kupeleka wanajeshi nchini Niger kurejesha utaratibu wa kikatiba ikiwa juhudi za kidiplomasia zitakwama.

“Suluhisho la kijeshi itakuwa janga,” Tajani aliwaambia waandishi wa habari alipowasili kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya katika mji wa Uhispania wa Toledo.

Amesema, “Tunatakiwa kufanya kazi siku baada ya siku kwa ajili ya suluhisho la kidiplomasia.”

Mzozo nchini Niger ni mmoja kati ya mada kuu za mkutano huo, ambayo itawasilishwa na Hassoumi Massoudou, waziri wa mambo ya nje wa serikali iliyoondolewa madarakani, na Omary Touray, mwenyekiti wa tume ya ECOWAS.

Tajani ameunga mkono pendekezo la Algeria wiki hii kutatua mzozo huo, kwa kuunda serikali ya mpito ya miezi sita inayoongozwa na raia.

Forum

XS
SM
MD
LG