Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 06:42

Italia yatolewa katika raundi ya kwanza.


Mabingwa watetezi Italia “The Azzuri Boys” wametolewa nje ya kombe la dunia baada ya kufungwa mabao 3-2 na Slovakia taifa dogo kuliko yote katika kombe la dunia mwaka huu.

Mabingwa watetezi Italia “The Azzuri Boys” wametolewa nje ya kombe la dunia baada ya kufungwa mabao 3-2 na Slovakia taifa dogo kuliko yote katika kombe la dunia mwaka huu.

Italia walipigana kufa na kupona katika dakika za mwisho lakini walikuwa wamechelewa mno. Mabao ya Slovakia katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji wao hatari Vittek mabao mawili na Kamil Kopunek kunako dakika ya 89 alifunga bao la tatu.

Kwa hiyo katika kundi F timu ya Slovakia na Paraguay zimefanikiwa kuingia raundi ya pili.

Nayo timu ya Cameroon wawakilishi wengine wa Afrika katika kundi E wameaga mashindano hayo kwa aibu bila hata ya pointi moja baada ya kufungwa na Uholanzi bao 2-1.

Na katika kundi hili hili la E Japan imeichabanga Denmark mabao 3-1 na hatimaye kufanikiwa kuwa timu ya pili ya Asia kuingia raundi ya pili ikiwa nyuma ya Uholanzi kutoka kundi hili.

Naye Rais Bill Clinton ameamua kubadili ratiba yake ya kuondoka Afrika Kusini ili aweze kujionea mechi ya Marekani na Ghana siku ya Jumamosi baada ya kufurahishwa na matokeo ya timu hiyo kuishinda Algeria na kuingia raundi ya pili.

XS
SM
MD
LG