Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:48

Israel yataja shambulio la mpakani kua ni la kigaidi


Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumapili ameyataja mauaji ya wanajeshi watatu yaliyofanywa na afisa wa idara ya usalama ya Misri kuwa shambulio la kigaidi na kuomba uchunguzi kamili wa pamoja na Cairo.

Misri imesema inashirikiana na Israel kuchunguza tukio hilo la Jumamosi.

Netanyahu aliliambia baraza lake la mawaziri katika hotuba kwa njia ya televisheni kwamba “Israel iliwasilisha ujumbe wa wazi kwa Serikali ya Misri. Tunatarajia kwamba uchunguzi wa pamoja utakuwa kamili na wa kina,”.

Maelezo zaidi kuhusu tukio hilo nadra kwenye mpaka yaliibuka Jumapili. Kwa kawaida kuna hali ya amani kwenye mpaka huo, kwani majirani wanashiriki ushirikiano wa karibu wa usalama, ingawa kuna ripoti za mara kwa mara za biashara ya magendo ya dawa za kulevya, ikiwemo biashara ya magendo iliyofanyika kabla ya mauaji hayo.

Jeshi la Israel limesema wawili kati ya wanajeshi wake waliuawa kwa kupigwa risase na afisa wa idara ya usalama ya Misri mapema Jumamosi, ambaye alivuka uzio wa mpaka.

Mpaka huo wa jangwani uko mbali na ilikchukua saa kadhaa kabla ya miili yao kupatikana.

Forum

XS
SM
MD
LG