Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 19:10

Israel yapuuzia sitisho la mapigano huko Gaza


Mfumo wa ulinzi wa makombora wa Iron Dome wa Israel unafyatua viunga kwenye roketi zilizorushwa kutoka Ukanda wa Gaza, huko Ashkelon, kusini mwa Israel. Jumamosi, Mei 13, 2023. (AP)

Israel siku ya Jumamosi ilipuuza sitisho la haraka la mapigano huko Gaza, ikisema kuwa jukumu lilikuwa kwa wanamgambo wa Kipalestina kuacha kurusha roketi

Israel siku ya Jumamosi ilipuuza sitisho la haraka la mapigano huko Gaza, ikisema kuwa jukumu lilikuwa kwa wanamgambo wa Kipalestina kuacha kurusha roketi kutoka kwenye ghala ya silaha ambapo lilipendekeza kuwa linaweza kuangamizwa ndani ya siku chache, huku ndege zake zikiendelea na mashambulizi katika eneo hilo.

"Hatufanyi mazungumzo ya kusitisha mapigano," Mshauri wa Usalama wa Taifa Tzachi Hanegbi alizungumza katika mkutano wa manispaa karibu na Jerusalem, na kuongeza kuwa kipaumbele cha juu cha Israel kwa sasa ni kuwashambulia wanamgambo hao.

Wapalestina wawili waliuawa katika uvamizi wa Israel kwenye viunga vya Nablus kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, ambapo mapigano yalizuka, Wizara ya Afya ya Palestina ilisema. Msemaji wa jeshi alisema watu wenye silaha walirushiana risasi na wanajeshi wa Israel.

XS
SM
MD
LG