Shirika rasmi la habari la Palestina, WAFA, Alhamisi limesema shambulizi la Israel la Beit Lahiya, kaskazini mwa Gaza, limeuwa takriban watu 11.
Jeshi la Israel limeripoti shambulizi la anga katika ghala la silaha karibu na eneo la jeshi la Hamas katika mji wa Gaza, pamoja na mashambulizi yaliyowauwa wanamgambo katikati mwa Gaza.
Duru nyingine ya mashambulizi ya anga yalilenga zaidi ya maeneo 10 kusini mwa Lebanon usiku kucha, jeshi la Israel limesema Alhamisi.
Mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran, jeshi la Israel limesema.
Forum