Jeshi la Israel liliandika kwenye mtandao wa X “ Wakati wa usiku ndege za kijeshi zilishambulia zaidi ya ngome 100 za Hamas katika Ukanda wa Gaza, na kuharibu mashimo ya handaki, maghala ya silaha na darzeni ya makao makuu ya operesheni zao.”
Hata hivyo, Israel imepanga kuondoka katika mji wa kaskazini wa Kiryat Shmona.
Maafisa wamesema Ijumaa kwamba wakazi wa mji huo watapelekwa kwenye hoteli kwa gharama za serikali.
Mji huo unapatikana karibu na mpaka kati ya Israel na Lebanon na umekuwa ukishambuliwa kwa maroketi na makombora kutoka makundi ya wanamgambo wa Palestina.
Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesafiri leo kuelekea Misri, ikiwa ziara yake ya hivi karibuni Mashariki ya Kati, wakati mzozo unazidi kupamba moto. Sunak tayari amekutana na viongozi wa Israel na mwanamfamle wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman.
Forum