Hatua hiyo ni sehemu ya operesheni ya mashambulizi ya ardhi na hewa, dhidi ya wanamgambo wa Hamas, kufuatia mashambulizi kusini mwa Israel wiki tatu zilizopita. Vikosi vya jeshi la Isreal la IDF vimesema kwamba ndege za kivita zimeharibu darzeni ya mahandaki, pamoja na kusambaratisha mfumo wa mawasiliano, uliopelekea takriban wakazi milioni 2.3 wa Gaza kukaribia kukatiza kabisa mawasiliano na ulimwengu.
Msemaji wa jeshi la Israel Rear Admiral Daniel Hagari wakati akizungumza na wanahabari mapema leo amesema kwamba, “Tunaendelea kupiga hatua kwenye vita, na usiku wa jana vikosi vya IDF viliingia Ukanda wa Gaza ukiwa mwendelezo wa operesheni ya ardhini.”
Ameongeza kusema kwamba vikosi hivyo vitaendelea kubaki huko , ikiashiria kwamba Israel huenda imeanza mashambulizi ya ardhini ndani ya Ukanda wa Gaza. Hagari pia ameongeza kusema kwamba Israel itaruhusu malori ya misaada yaliobeba chakula, maji na dawa kuingia huko Gaza.
Forum