Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 03, 2024 Local time: 23:06

Israel na Hamas wanakaribia makubaliano ya kuachiliwa mateka huko Gaza


Benjamini Netenyahu, Waziri Mkuu wa Israel
Benjamini Netenyahu, Waziri Mkuu wa Israel

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewaambia wanajeshi wa akiba  “Tunapiga hatua. Sidhani kama ni muhimu kusema sana, sio kwa  wakati huu, lakini natumaini kutakuwa na habari njema hivi karibuni

Israel na Hamas zimeashiria leo Jumanne kwamba makubaliano yanakaribia kukamilika ya kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo huko Gaza, ingawa maelezo ya makubaliano hayo hayana uhakika.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewaambia wanajeshi wa akiba “Tunapiga hatua. Sidhani kama ni muhimu kusema sana, sio kwa wakati huu, lakini natumaini kutakuwa na habari njema hivi karibuni.

Mkuu wa Mamlaka ya Masuala ya Wafungwa wa Palestina, Qaddoura Fares, alisema “makubaliano ya kubadilishana wafungwa yanajumuisha kuachiliwa kwa watoto 350 na wanawake 82 wa Kipalestina” wanaoshikiliwa na Israel.

Kwa siku kadhaa, taarifa za habari za Marekani zimesema takriban wanawake 50 na watoto kati ya watu 240 waliokamatwa na wanamgambo wa Hamas wakati wa shambulio la kushtukiza la Oktoba 7 kwa Israel wanaweza kuachiliwa huru.

Aidha sitisho la mapigano la siku tano linaweza kutekelezwa, lakini sio makubaliano ya kusitisha kabisa mapigano ambayo baadhi ya viongozi wa dunia wanatoa wito kwa hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG