Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 12:04

Netanyahu asitisha misaada kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa


waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika mkutano na baraza la mawaziri mjini Jerusalem Desemba 25, 2016.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema Jumapili katika mkutano na baraza lake la mawaziri kwamba serikali za Israel na Marekani zimekubaliana kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa sio mahala pa kutatua matatizo ya upanuzi wa makaiz ya waisraeli huko Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki.

Lakini azimio lililopitishwa dhidi ya ujenzi wa makazi ya waisrael siku ya Ijumaa katika baraza la usalama liliridhiwa na Marekani bila ya kutumia kura yake ya turufu kulizuia.

Netanyahu alisema Jumapili amezungumza na "marafiki zetu nchini Marekani, pande zote warepublican na wademokrat," ambao "wanaelewa namna azimio hilo lilivyokuwa siyo la busara."

Amesema anategemea kushirikiana na hawa marafiki na "utawala mpya utakaochukua madaraka mwezi ujao." Rais mteule ataanza kazi rasmi januari 20.

Waziri mkuu amesema hivi karibuni alimueleza waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John kerry kuwa "rafiki hawapeleki marafiki zao kwenye baraza la usalama."

Kutokana na kukasirishwa kwake na kura iliyopigwa kwa azimio hilo la baraza la usalama, Netanyahu ametoa amri kwa serikali yake kusitisha misaada kwenye mashirika matano ya Umoj awa Mataifa.

katika maelezo yaliyotolewa katika televisheni Jumapili, waziri mkuu huyo amesema agizo lake alilolitoa hivi sasa linazuia takriban dola milioni 8 kufadhili mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo hakuyataja, na akasema, "yako mengi yatakayojitokeza." Lakini hakutoa ufafanuzi zaidi.

Wakati huo huo Netanyahu alielezea masikitiko yake juu ya serikali ya Marekani na kumshutumu rais Barack Obama kwa kuacha kutekeleza ahadi ya kuisaidia Israel.

"uamuzi wa Obama siyo tu hausaidii kuleta amani, lakini ni kikwazo cha kufikia amani," amesema.

Aliyekuwa mmoja wa wapatanishi wa mazungumzo ya amani upande wa wapalestina, Saeb Erekati ameiita kura ya azimio la Umoja wa Mataifa "ni ujumbe wa pamoja na uliowazi" kwa Netanyahu kwamba sera zake haziwezi kuleta amani na usalama siyo tu ndani ya Israel lakini hata sehemu nyingine katika Mashariki ya Kati.

Shirika la habari la Ufaransa (AFP) limemnukuu msemaji wa Hamas akisema anawashukuru wanadiplomasia waliopiga kura kupitisha azimio hilo.

Fawzy Barhoum ameielezea kuwa hiyo kama "kura ya kulinda haki za wapalestina katika ardhi yao."

XS
SM
MD
LG