Mkuu wa shirika la kimataifa kuhusu nguvu za nuclear Rafael Grossi, ameitembelea Israel ambayo imekuwa ikiishutumu Iran kwa kutengeneza silaha za nuclear na inaunga mkono kurudia mkataba wa nuclear wa mwaka 2015 kati ya Iran na nchi nyingine zenye nguvu duniani.
Bennett ameelezea wasiwasi kuhusu hatua ya Iran kuendelea kutengeneza nguvu za nuclear huku ikisema uongo kwa jumuiya ya kimataifa na kueneza habari potofu.
Amesisitiza umuhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka dhidi ya Iran kwa kutumia nguvu zote ili kuizuia kuendelea kutengeneza nguvu za nuclear.
Israel inaaminika kuwa nchi pekee yenye silaha za nuclear katika mashariki ya kati lakini haijawahi kusema hadharani kwamba inamiliki silaha hizo.