Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 22:12

Israel imeongeza mashambulizi Ukingo wa Magharibi


Familia za Kipalestina zikikimbia kufuatia mashambulizi ya Israel katika kambi ya Nur Shams karibu na mji wa Tulkarem Agosti 28, 2024, katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Ukingo wa Magharibi.
Familia za Kipalestina zikikimbia kufuatia mashambulizi ya Israel katika kambi ya Nur Shams karibu na mji wa Tulkarem Agosti 28, 2024, katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Ukingo wa Magharibi.

Israel  leo imeendelea kutekeleza mashambulizi ya kijeshi katika  eneo la Ukingo wa Magharibi libalokaliwa kimabavu, ikisema kwamba inalenga kuyavunja  kabisa makundi ya wanamgambo na kuzuia  ongezeko la mashambulizi dhidi ya wa Israel.

Shirika la mwezi mwekundu limesema kwamba watu watatu wamefariki kufuatia shambulizi dhidi ya gari, nje ya Tulkarem.

Bila kutoa taarifa zaidi, jeshi la Israel limethibitisha kwamba limetekeleza shambulizi hilo.

Wapalestina wamesema kwamba operesheni kama hiyo inalenga kuipatia Israel uwezo wa kutawala sehemu hiyo kijeshi.

Wakati huo huo, walowezi wa kiyahudi wameongeza mashambulizi dhidi ya wapalestina.

Jeshi la Israel liliesema jana Jumatano kwamba limeongeza mashambulizi katika mji wa Tulkarem, Ukingo wa Magharibi, na katika miji mingine miwili ya kaskazini.

Limesema kwamba limeharibu maabara ya kutengeneza vilipuzi, karakana ya kutengeneza silaha na gari lililokuwa limejaa vilipuzi.

Jeshi la Israel pia limesema kwamba shambulizi la anga limeuwa wapiganaji watano katika mji wa Tubas.

Forum

XS
SM
MD
LG