Mji wa Khan Yunis upande wa kusini wa Ukanda wa Gaza umeshambuliwa kwa mfululizo wa mabomu kutoka jeshi la Israel tangu kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda siku ya Ijuma kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.
Kulingana na shirika la habari la Associate Press, Israel imetoa onyo kwa wakazi wa kusini mwa gaza kuhama baada ya kukimbia kutoka maeneo ya kaskazini, inapobadili mkakati wake wa mashambulizi kuelekea upande wa kusini, ambako inadai viongozi wa Hamas wamejificha.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema jumamosui kwamba kampeni ya mashambulizi itaendelea hadi mateka walochukuliwa na Hamas hapo Oktoba 7 wamerudishwa na kundi la Hamas limeangamizwa.
“Vita vikali vitarajiwe siku za mbele,” alisema Netanyahu.
Makamu rais wa Marekani, Kamala Harris alisema Jumamosi kwamba “Wapalestina wengi wasio na hatia wameuliwa.” Akizungumza kwenye mkutano wa hali ya hewa COP 28 mjini Dubai, amesema “kwa hakika kiwango cha maafa kikachowakumba raia na picha na video kutoka Gaza ni za kusikitisha sana.”
Karibu wapalestina 200 wameuliwa tangu kuvunjika kwa makubaliano kati ya Hamas na Israel siku ya Ijuma, na hivo kuongeza kiwango cha vifo kufikia 15 523 tangu kuanza mapigano ya Oktoba huko Gaza kulingana na wizara ya afya ya Gaza na watu wengine elfu 40 wamejeruhiwa, na kwamba asili mia 70 kati yao ni wanawake na watoto.
Forum