Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:33

20 wauwawa kwa bomu Mogadishu, Somalia


Maafisa wa Usalama wanamsaidia mbunge wa Somalia Abdalla Boss aliyejeruhiwa wakati mtu aliyekuwa kwenye gari alilipua bomu karibu na makao ya rais mjini Mogadishu Jumanne tarehe 30, Agosti, 2016.
Maafisa wa Usalama wanamsaidia mbunge wa Somalia Abdalla Boss aliyejeruhiwa wakati mtu aliyekuwa kwenye gari alilipua bomu karibu na makao ya rais mjini Mogadishu Jumanne tarehe 30, Agosti, 2016.

Bomu lililotegwa kwenye gari lililipuka katika makao ya rais wa Somalia kwenye mji mkuu wa Mogadishu na kuua takriban watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30 siku ya Jumanne. Hayo ni kulingana na maafisa wa usalama nchini Somalia.

Mlinzi mmoja wa rais wa Somalia ambaye hakutaka jina lake litajwe, ameimbia Sauti ya Amerika kuwa mtu aliyekuwa anaendesha gari kwa kasi alianza kufyatua risasi na ikabidi walinzi kumfyatulia risasi pia. Hatimaye dereva huyo alisimamisha gari lake na kulipua bomu lililokuwemo.

Gari hilo liligonga ukuta wa hoteli iiitwayo SYL iliyo karibu na uwannja wa makao ya rais, Villa Somalia. Baadhi ya waliojeruhiwa ni pamoja na mawaziri wawili wa serikali ya Somalia, wabunge wawili na waandishi wawili wa habari, ambao wote walikuwa kwenye hoteli hiyo wakati mlipuko huo ulitokea. Wanamgambo wa Al-Shabaab mara kwa mara hushambulia mahoteli mjini Mogadishu, hususan kwa sababu ndiko maafisa wa serikali hufanya mikutano yao. Kundi hilo lilivamia hoteli hiyo ya SYL mwezi Februari na kuwaua takriban watu tisa.

XS
SM
MD
LG