Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 27, 2025 Local time: 13:37

Iran yakamilisha zoezi kubwa zaidi la kijeshi


Vifaru vya jeshi la Iran vikiwa kwenye mazoezi. Picha ya AP Feb 22, 2025.
Vifaru vya jeshi la Iran vikiwa kwenye mazoezi. Picha ya AP Feb 22, 2025.

Iran imekamilisha  miezi miwili ya mazoezi makali ya kijeshi katika miongo kadhaa huku ikijaribu kuzuia uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa mahasimu wake Israel na Marekani, watafiti wa usalama wameiambia VOA.

Watafiti hao wenye makao yao mjini Washington pia wanasema mazoezi hayo ya Iran yalianza mwishoni mwa Disemba, na yalitarajiwa kukamilika katikati ya mwezi Machi, yakihusisha baadhi ya mifumo ya silaha ambazo ni tishio kwa Marekani na Israel huku mengine yakifichua udhaifu katika uwezo wa Iran wa kujilinda.

"Kasi, nguvu na utangazaji wa mazoezi hayo hayajawahi kutokea," Behnam Ben Taleblu wa Wakfu wa Ulinzi wa Demokrasia amesema. Farzin Nadimi kutoka Taasisi ya Washington ya Sera za Mashariki amesema amekuwa akisomea masuala ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu kwa muda wa miaka 20 iliyopita."Sijawahi kuwaona wakifanya mazoezi mengi kwa muda mfupi hivyo kama ilivyo shuhudiwa," alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG