Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:27

Iran yakamata meli iliyokuwa inasafirisha mafuta


Meli ya kusafirisha mafuta ya Iran. May 25, 2020.
Meli ya kusafirisha mafuta ya Iran. May 25, 2020.

Maafisa wa Iran wamekamata meli iliyokuwa inajaribu kusafirisha mafuta kwa njia haramu kutoka nchini humo, na kuwazuilia wafanyakazi wake.

Iran, ambayo ina mafuta ya bei nafuu kote duniani kutokana na gharama ya chini kwa wasafirishaji, pamoja na kushuka kwa thamani ya sarafu yake, imekuwa ikikumbana na biashara haramu ya mafuta kupitia baharini kuelekea ghuba ya kiarabu.

Meli hiyo ilikuwa imebeba lita 550,000 za mafuta, na ilikamatwa katika maji ya ghuba.

Imesafirishwa hadi katika bandari ya Hormozgan, kusini mwa nchi.

Uchunguzi unafanyika kabla ya kutoa taarifa zaidi.

Meli kadhaa zimekamatwa katika miezi ya hivi karibuni, zikisafirisha mafuta kutoka Iran kwa njia haramu.

XS
SM
MD
LG