Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:50

Iran yaionya Ufaransa


Iran iliionya Ufaransa Jumatano baada ya jarida la kejeli la Charlie Hebdo kuchapisha katuni zinazomoonyesha kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei ambazo Tehran iliziona kuwa za kashfa.

Jarida hilo la kila wiki lilichapisha katuni kadhaa za kumkejeli kiongozi huyo wa juu kabisa wa kidini na kisiasa katika jamhuri ya Kiislamu kama sehemu ya shindano lililoanzishwa mwezi Disemba kuunga mkono vuguvugu la maandamano lililodumu kwa miezi mitatu.

"Kitendo cha matusi na aibu cha uchapishaji wa Kifaransa katika kuchapisha katuni dhidi ya mamlaka ya kidini na kisiasa hakitapita bila jibu," Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian aliandika katika ujumbe wa Twitter.

Baadaye Jumatano, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilisema kuwa imemwita balozi wa Ufaransa Nicolas Roche.

XS
SM
MD
LG