Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 02:31

Iran: Wanajeshi wanne wa kikosi cha usalama wauawa katika shambulio la kigaidi


Kamanda wa kikosi cha usalama cha Iran Jenerali Hossein Salami, akizungumza kwenye mazishi huko Shiraz, Oktoba 29, 2022. Picha ya Reuters

Shirika la habari la serikali ya Iran (IRNA) leo Jumatatu limeripoti kwamba shambulio la kigaidi limeua wanajeshi wanne wa kikosi cha usalama cha Iran kusini mashariki mwa nchi.

Wanajeshi hao wa kikosi cha The Islamic Revolutionary Guard waliuawa “katika kitendo cha ugaidi” kwenye eneo la Saravan katika jimbo la Sistan-Baluchistan karibu na mpaka wa Pakistan, IRNA imesema.

Eneo hilo ni mojawapo ya eneo maskini la Iran na makazi kwa Wabaluchstani walio wachache, ambao ni waumini wa kiislamu wa dhehebu la suni badala ya dhehebu la Shia lenye waumini wengi nchini Iran.

Awali, eneo hilo lilishuhudia mapigano na magenge yanayofanya biashara ya magendo ya dawa za kulevya pamoja na waasi kutoka makundi ya wachache wa kabila la Baluchi na makundi ya waislamu wenye itikadi kali wa dhehebu la Suni.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG