Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 06:59

Iran ina matumiani ya kufikia makubaliano ya nuklia na mataifa makuu


Wajumbe wa mataifa 6 kuu za dunia na Iran kwenye mazungumzo ya Uswisi
Wajumbe wa mataifa 6 kuu za dunia na Iran kwenye mazungumzo ya Uswisi

Waziri wa masuala ya nchi za nje wa Iran Mohammed Zarif, alikuwa na matumaini mazuri kuhusiana na mpango wa mkataba ulofikiwa huko Uswisi, April 2, ambao utapunguza mradi wa nuklia wa Iran na kuondowa vikwazo vya kimataifa.

Anasema pande zote zitafanya kazi bila kusita hadi kufikia makubaliano ya mwisho ifikapo Juni 30 na kwamba Iran ina dhamira ya dhati ya kukamilisha utaratibu huo.

Baraza la Usalama la Umoja Mataifa limeweka mara nne vikwazo dhidi ya Iran tangu mwaka 2006 kwa mradi wake wa nuklia, ambao nchi sita zenye nguvu duniani zinaamini unaweza kutumiwa kwa minajili ya kijeshi.

Japo kuna baadhi ya watu huko Tehran wanaopinga mkataba huo, wakisema unazipatia nchi za Magharibi ruhusa ya kuingia maeneo ya kijeshi, lakini Zarif anasema serikali yake iko tayari kutekeleza Itifaki ziada ya mkataba wa kimataifa wa kutoeneza nuklia ili kusaidia kuongeza imani ya nchi za magharibi. Iran daima imekana kuwa inataka kutengeneza bomu la nuklia na inasema inataka kuwa na mpango wa nuklia kwa matumizi ya Amani pekee.

Zarif anasema iwapo mkataba wa Juni 30 utaafikiwa, basi anataraji kwamba Baraza la Usalama la Umoja Mataifa litapitisha azimio jipya katika siku zitakazofwatia, kuunga mkono mkataba huo na kuanza utaratibu wa kuondowa vikwazo.

Kumekuwepo na upinzani mdogo kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Marekani kuhusiana na mkataba wa Iran na kuondolewa kwa vikwazo. Wanasema,Tehran haiwezi kuaminiwa kwa sababu ya vitisho vyake dhidi ya Israel na uungaji mkono wake hapo awali wa makundi ya kigaidi.

Zarif anasema Marekani inalaizmika kuheshimu sharia za kimatiafa kufwata makubaliano ambayo utwala wa Obama utatia saini.

Vile vile, alimkosowa kongozi wa Israel Benjamin Netanyahu, kwa msimamo wake wa daima dhidi ya mpango wa nuklia wa Iran.

XS
SM
MD
LG