Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:34

Iran imewahukumu wanaume 7 na mwanamke mmoja; inaripoti Mizan


Bendera ya Iran

Hukumu hiyo inakuja kabla ya maadhimisho ya mwaka mmoja ya kifo cha Amini hapo Septemba 16 wakati mamlaka zimekuwa zikiwakamata wanaharakati na watu wengine katika jaribio la wazi la kukandamiza upinzani wowote kabla ya hukumu hiyo

Iran imewahukumu wanaume saba na mwanamke mmoja kifungo baada ya kukutwa na hatia ya kuwasaidia wanaume wawili ambao awali walinyongwa kwa kumuua mwanajeshi wa kujitolea wakati wa maandamano ya nchi nzima mwaka jana yaliyofuatia kifo cha Mahsa Amini akiwa mikononi mwa polisi, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti Jumatano.

Hukumu hiyo inakuja kabla ya maadhimisho ya mwaka mmoja ya kifo cha Amini hapo Septemba 16 wakati mamlaka zimekuwa zikiwakamata wanaharakati na watu wengine katika jaribio la wazi la kukandamiza upinzani wowote kabla ya hukumu hiyo.

Ripoti hiyo ya shirika la habari la Mizan ilitoa uthibitisho rasmi wa kwanza wa hukumu hiyo iliyotolewa mapema na mahakama ya mapinduzi katika mji wa Karaj ambako mauaji ya Novemba yalitokea. Ripoti hiyo ilisema Mahakama Kuu nchini humo iliunga mkono hukumu iliyotolewa kufuatia rufaa ya mawakili wa wale waliohukumiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG