Iran imesindika idadi kubwa ya madini ya uranium, ikiongeza shehena yake hadi kukaribia kiwango cha utengenezaji silaha, shirika la Umoja wa Mataifa la kufuatilia silaha za nyuklia limesema Jumatatu katika ripoti ya siri.
Ripoti hiyo, iliyoonekana na shirika la habari la Associated Press, imesema usambazaji wa madini ya uranium ya Iran umefikia mara 30 zaidi ya kiwango kilichokubaliwa katika makubaliano ya mwaka 2015, kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu duniani ili kupunguza program ya nyuklia ya Iran.
Kiwango cha hifadhi ya uranium kilichorutubishwa nchini Iran, ni zaidi ya kilo 6,201.3 ikiwa ni ongezeko la kilo 675.8 tangu ripoti ya mwisho ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki ya mwezi Februari. Rafael Grossi, mkurugenzi wa IAEA na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti silaha za nyuklia, alionya mwezi uliopita kwamba Iran imekuwa na uranium iliyorutubishwa yenye kiwango cha kutosha kwa mabomu kadhaa ya nyuklia iwapo itaamua kutengeneza.
“Kiwango cha ukaguzi nchini Iran hakiko katika kiwango ambacho tunapaswa kuwa nacho”, Grossi aliiambia Sky News mwezi April. Maafisa wa Iran wametishia huenda wakatumia silaha za atomiki. Iran imesema program yake ya nyuklia ni ya amani.
Forum