Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:26

Iran imefanya mauaji ya pili ya mfungwa anayehusishwa na maandamano


Iran imetekeleza mauaji ya pili ya mfungwa aliyehusishwa na maandamano yaliyoanza Septemba
Iran imetekeleza mauaji ya pili ya mfungwa aliyehusishwa na maandamano yaliyoanza Septemba

Wanaharakati wanasema Iran imewahukumu watu wasiopungua darzeni moja kunyongwa hadi kufa katika vikao vya faragha. Mtu wa kwanza aliyeuawa kuhusiana na maandamano hayo aliuawa wiki iliyopita

Iran siku ya Jumatatu ilisema ilitekeleza mauaji yake ya pili ya mfungwa anayehusishwa na maandamano ya nchi nzima yaliyoanza mwezi Septemba.

Shirika la habari la Mizan linaloendeshwa na mahakama ya Iran limesema Majidreza Rahnavard alinyongwa hadharani siku ya Jumatatu katika mji wa Mashhad.

Rahnavard alishtakiwa kwa kuwadunga kisu wanachama wawili wa kikosi cha usalama mwezi uliopita huko Mashhad.

Wanaharakati wanasema Iran imewahukumu watu wasiopungua darzeni moja kunyongwa hadi kufa katika vikao vya faragha.

Mtu wa kwanza aliyeuawa kuhusiana na maandamano hayo aliuawa wiki iliyopita.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema anatarajia mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya kuidhinisha "mfuko mgumu sana wa vikwazo" dhidi ya Iran kwa ukandamizaji wake dhidi ya waandamanaji na jukumu lake la kusambaza ndege zisizo na rubani ambazo Russia imetumia kuishambulia Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amewaambia waandishi wa habari kabla ya mkutano huo mjini Brussels kwamba mauaji ya Iran ni jaribio la wazi la vitisho.

XS
SM
MD
LG