Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:50

Ajali ya treni iliyoua 150 India yaendelea kuzua maswali


Treni iliyoangunga nchini India na kuwaua takriban abiria 150. Ajali hiyo imezua maswali chungu nzima huku wataalam wakijaribu kutadhimini kilichoisababisha.
Treni iliyoangunga nchini India na kuwaua takriban abiria 150. Ajali hiyo imezua maswali chungu nzima huku wataalam wakijaribu kutadhimini kilichoisababisha.

Watu 150 wamekufa na takribani 200 wamejeruhiwa kwenye ajali ya treni iliyotokea huko India mwishoni mwa wiki.

Ajali hii iliyosababisha vifo vya watu wengi katika kipindi cha miaka 17 inaangaliwa kama moja ya nguzo ya ukosoaji mbaya uliopo kwenye miundo mbinu na teknolojia katika mfumo wa reli na kuzua maswali kuhusu juhudi za kuboresha usalama kwenye mtandao ambao unahudumia takribani watu milioni 23 kila siku.

Chanzo halisi cha ajali hiyo bado hakijajulikana. Waziri wa usafiri Manoj Sinha alisema ajali hiyo huwenda imesababishwa na kukatika kwa njia ya reli. Reli hukatika wakati kunapotokea michubuko midogo midogo ya muda mrefu ambayo hupelekea kuwa mikubwa na kuachana.

Hata hivyo maafisa wanasema njia ambayo ajali hiyo imetokea ilifanyiwa ukaguzi na kuonekana kuwa katika hali nzuri kabla ya ajali hiyo kutokea.

XS
SM
MD
LG