Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 19:06

India Bado Yakabiliana na Joto Kali


India inasubiri kuanza kwa msimu wa mvua wa kila mwaka wa Monsoon kumaliza wimbi la joto kali ambalo mpaka sasa limeshaua zaidi ya watu 2,200 katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo.

Manyunyu ya mvua pamoja na radi zilitokea kusini mwa India, jana Jumapili na kuleta ahueni kubwa.

Pamoja na hali hiyo maafisa wamesema joto kali bado linaweza kuendelea kwa siku nyingine katika majimbo ya Andhra Pradesh, na Telangana.

Kipindi cha mchana joto lilifika kwenye kipimo cha Sentigredi, kati ya 45 na 47 sawa na Faranhaiti, 113 na 116 mwishomi mwa juma.

Katika jimbo la Andhra Pradesh imeripotiwa zaidi ya vifo 146 siku ya Jumamosi, na kusababisha kuongezeka kwa vifo kufikia 1,636 katika jimbo hilo peke yake.

XS
SM
MD
LG