Mkurugenzi mtendaji wa shirika la fedha la kimataifa-IMF ameidhinisha Jumatatu tathmini ya kwanza ya mpango wa ufuatiliaji wa wafanyakazi wa Sudan-SMP lakini alitaka mageuzi ya viwango vya ushuru wa forodha na uwazi zaidi juu ya biashara zinazomilikiwa na serikali.
Mamlaka za Sudan zimefanya maendeleo ya msingi katika kuweka rekodi nzuri ya utekelezaji wa sera na mageuzi, hitaji muhimu ambalo hatimaye limezaa matunda ya kupata ahueni ya deni ilisema taarifa ya IMF ikitoa mfano wa kushuka kwa thamani ya sarafu na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta.
IMF ilionya kuwa hali ya uchumi bado ni tete nchini Sudan ambapo mzozo mkubwa wa uchumi umesababisha mfumuko wa bei hadi asilimia 300 na uhaba wa bidhaa za msingi.