Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:06

IMF imepitisha mkopo wa dola milioni 447 kwa Kenya


Logo ya shirika la fedha la kimataifa (IMF).
Logo ya shirika la fedha la kimataifa (IMF).

Kenya ilifikia makubaliano ya ufadhili wa miezi 38 na IMF mwezi April mwaka 2021 chini ya ufadhili wake wa ziada na mkopo ulioongezwa wa utoaji fedha wa karibuni unaleta jumla ya dola bilioni 1.65 hadi sasa

Bodi ya Shirika la fedha la kimataifa (IMF) imepitisha mkopo wa dola milioni 447 kwa Kenya baada ya kutathmini program zake za mikopo. Deni la umma la kenya lilikuwa limeanza kupungua kutokana na maendeleo ya kuchanganyisha pamoja sera zake za fedha, IMF imesema katika taarifa yake na kuongeza kuwa imetenga fedha za ziada chini ya wizara iliyopo.

Taifa hilo la Afrika mashariki lilifikia makubaliano ya ufadhili wa miezi 38 na IMF mwezi April mwaka 2021 chini ya ufadhili wake wa ziada katika mkopo ulioongezwa. Utoaji wa fedha wa karibuni unaleta jumla ya dola bilioni 1.65 hadi sasa.

Kenya hivi sasa itapata zaidi ya dola bilioni mbili chini ya mpango wa sasa IMF imesema. Pande zote zimekubali kwamba ongezeko la mwezi uliopita kwa ajili ya mahitaji ya kifedha ni kutokana na ukame na changamoto za hali ya kifedha duniani.

Serikali ya Rais Ruto ambayo imeingia madarakani mwezi septemba mwaka 2022 ina mpango wa kupunguza gharama za ukopaji wa kibiashara kwa kubadilishana na vyanzo rahisi kama vile benki ya duniani ili kupunguza shinikizo la deni kukidhi mapato.

XS
SM
MD
LG