Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:21

Idara ya upelelezi Afghanistan yathibitisha kifo cha Mansoor


Gazeti moja likieleza taarifa za kiongozi wa Taliban, Mullah Akhtar Mansour. Dec. 6, 2015.
Gazeti moja likieleza taarifa za kiongozi wa Taliban, Mullah Akhtar Mansour. Dec. 6, 2015.

Idara ya upelelezi ya Afghanistan imethibitisha kwamba kiongozi wa Taliban, Mullah Akhtar Mansoor aliuwawa katika shambuylizi moja la anga la Marekani nchini Pakistan karibu na mpaka na Afghanistan.

Pakistan ilisema iliarifiwa na Marekani baada ya shambulizi la ndege zisizotumia rubani yaani drone kufanyika lakini iliikosoa Washington kwa kukiuka uhuru wake. Islamabad haikuthibitisha mara moja kwamba Mansoor aliuwawa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alisema Jumapili wakati wa safari yake kuelekea Mynmar kwamba Mansoor alikuwa mlengwa kwa sababu ni tishio kubwa kwa wanajeshi wa Marekani, raia wa Afghanistan na vikosi vya usalama vya Afghanistan na kwamba Mansoor alipinga moja kwa moja mashauriano ya amani.

Maafisa wa Taliban wamethibitisha kwa siri kifo cha kiongozi wao lakini hawakuwa tayari kutajwa wakisema uamuzi wowote wa mwisho utafanywa na kundi linaloitwa Rahbari au kamati ya uongozi.

Shambulizi la drone lilitokea Jumamosi huko Dalbandin, katika jimbo la Baluchistan kwa mujibu wa shirika la kipelelezi la Afghanistan-NDS.

XS
SM
MD
LG