Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 15:14

Interpol yataka taarifa za watu 11 kwa mashitaka ya usafirishaji watu


Idara ya Interpol mapema leo Alhamisi imetoa wito kwa umma kusaidia kutafuta watu 11 wanaomanika kuwa walanguzi haramu wa binadamu.

Idara hiyo ya kimataifa yenye makao yake Ufaransa tayari imewakamata watu 26 kutoka mataifa mbali mbali wanaoshutumiwa kuhusika kwenye usafirishaji haramu wa binadamu.

Interpol imechapisha picha za watu hao 11 kwenye tovuti lake mapema leo wito ukitolewa kwa yeyote mwenye habari kujitokeza ingawa huwa ni vigumu kwa kuwa walioathirika mara nyingi wanahofia kutoa habari.

Kulingana na Interpol, washukiwa wa usafirishaji haramu wa binadamu hujipatia maelfu ya dola kutoka kwa kila mmoja wanaenuia kupeleka Ulaya.

Kuna kisa cha kundi moja kutoka Albania lililokuwa likiitisha dola 16,000 kwa kila mtu ili kuvushwa kwa boti kutoka Ufaransa hadi Uingereza.

XS
SM
MD
LG