Ripoti imegundua kwamba migogoro ya Sudan, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwenye ardhi za Wa-Palestina imesababisha karibu theluthi mbili ya waliokoseshwa makazi kutokana na ghasia ambazo zimesambaa katika nchi 66 hapo mwaka 2023.
“Mnamo miaka miwili iliyopita, kumekuwa tukiona viwango vipya vya kushtusha vya watu wanaokimbia nyumba zao kutokana na migogoro na ghasia, hata katika maeneo ambayo yemeshuhudia mabadiliko mazuri,” amesema mkurugenzi wa IDMC, Alexandra Bilak.
Katika taarifa iliyotolewa wakati mmoja na repoti iliyochapishwa Jumanne , amesema kuwa mamilioni ya watu waliolazimishwa kukimbia katika kipindi cha mwaka 2023 walikuwa ni “sehemu ndogo ya tatizo kamili.”
Katika repoti yake ya 2023, idadi ya watu waliolazimishwa kuyahama makazi yao, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limeripoti kuwa watu milioni 62.5 walipoteza makazi yao ilipofika mwishoni mwa mwaka 2022 ikilinganishwa na wakimbizi waliokimbia migogoro na ghasia na ukatili mwaka huo.
Forum