Takriban nusu ya wabunge nchini Kenya wanatarajiwa kuhama kwenye vyama vyao na kujiunga na vyama vingine vya siasa wakati wakiomba kuchaguliwa tena katika uchaguzi ujao wa Agosti.
Kabla ya tarehe ya mwisho ya Machi 26 kwa vyama kuwasilisha orodha ya wanachama wao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kiasi cha wanachama 180 wa Bunge la Taifa na Baraza la Seneti wametangaza hadharani kuhama katika vyama vilivyowadhamini katika uchaguzi wa 2017, huku idadi hiyo ikitegemewa kuongezeka
Tayari kuna wanachama 416 katika mabunge mawili ya taifa, ikiwemo wale walioteuliwa kuwakilisha makundi maalum kama vile vijana, wanawake na watu wenye kuishi na ulemavu.
Kuhama kwa idadi kubwa ya wanachama hakujaiacha serikali za ugatuzi, huku sio chini ya magavana wa Kaunti 15 kati ya 26 wa awamu ya kwanza ambao wanatakiwa kuchaguliwa tena mwaka huu wamebadilisha ushirika wao na chama.
Kwa mujibu wa sheria mpya iliyopitishwa Februari, wagombea kwa nafasi mbalimbali za kuchaguliwa lazima wathibitishe uanachama wao wa chama ifikapo Machi 26 ili kuweza kukidhi uhalali wa kugombea katika uchaguzi wa awali wa chama mwezi Aprili.
Sheria hiyo inawaruhusu wale ambao hawana mafungamano na chama cha siasa kugombea kwa nafasi binafsi.
Wengi kati ya wanasiasa wanaohama kwenda vyama vipya wanaona tiketi mbadala ya kugombea inawapa fursa nzuri zaidi ya kushinda.
Kadhalika, baadhi hawana imani kuwa vyama vyao vita endesha uchaguzi wa awali wa haki. Kuhama kwao katika msimu huu kunaonyesha nchi inavyohangaika na demokrasia ya vyama vingi. Hakuna rais aliyegombea au kutetea nafasi yake kwa kutumia chama kile kile au muungano ule ule kwa chaguzi nne zilizopita.
Wakenya watapiga kura katika uchaguzi wa saba katika kipindi cha miaka 30 tangu kuanzishwa tena kwa mfumo wa siasa za vyama vingi.
Nchi hiyo ilikuwa imetangazwa kuwa ni taifa la chama kimoja mwaka 1982. Lakini, miaka iliyofuatia, vyama vya siasa ambavyo vimejitokeza kwa ajili ya kipindi cha uchaguzi vimeonekana kuwa dhaifu kwa kukosekana shinikizo la maadili, kama vile soko huru na itikadi mbalimbali za kisoshalisti.
Vyama vinne vikuu katika uchaguzi mkuu wa 1992 – Kanu, Ford Kenya, Ford Asili na chama cha Demokratik – ni kivuli kile cha vyama vile vile vilivyokuwa awali.
Kanu, chama cha tangu uhuru, na kilichoshinda viti 100 vya bunge mwaka 1992 chini ya uongozi wa rais Daniel Arap Moi, hivi sasa kina viti 10 tu katika Bunge la Taifa lililoongezeka.
Ford-Kenya ni chama pekee kingine katika kizazi kilichotangulia, nacho kimeshuhudia kupungua kwa idadi ya viti vyake bungeni kutoka 31 mwaka 1992 hadi 12 hivi sasa.
Hivi karibuni, vyama vya siasa vimejikuta vikihangaika kujitambulisha, kwa sababu ya kuongezeka muungano wa vyama – kwa kiwango kikubwa ushirikiano wa kikabila kwa haraka wakijikusanya kama chombo chenye lengo la kushinda uchaguzi.
Wengi wao kati ya wale wanaohama vyama hivi sasa wanabadilisha mahusiano yao ima kwenda chama cha muungano wa Azimio la Umoja linalohusishwa na Rais Uhuru Kenyatta na mrithi wake anayetakiwa, Raila Odinga, au chama cha Kenya Kwanza Alliance kinachoongozwa na Makamu wa Rais William Ruto.
Muungano wa pande hizo mbili umefanyika katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African, Kenya.