Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:47

Idadi ya wanaofariki wakikimbilia Ulaya yaongezeka maradufu - UNHCR


Balozi wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Filippo Grandi.
Balozi wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Filippo Grandi.

Zaidi ya wakimbizi, wahamiaji na waomba hifadhi 3,000 wamekufa au hawajulikani walipo, mwaka 2021 wakati wakijaribu kufika Ulaya kupitia Bahari ya Mediterranean na Bahari ya Atlantic, shirika la kuhudumia wakimbizi limesema katika ripoti yake Ijumaa.

Ripoti hiyo inaonyesha idadi ya waliokufa ni kubwa katika miaka ya hivi karibuni.

Maelfu ya Waafrika wanatumia njia ndefu na hatari kufika Ulaya kila mwaka mara nyingi wakipitia Jangwa la Sahara na kuacha ufukwe wa Afrika Kaskazini wakiwa kwenye boti ndogo wakikimbia hali ngumu au kutafuta maisha bora.

Mwaka 2021, UNHCR iliripoti watu 3,077 walikufa au hawajulikani walipo, karibu mara mbili ya idadi ya mwaka 2020.

UNHCR ilianza kutoa idadi mwaka 2019 na idadi ya watu wanaopoteza maisha inaongezeka kila mwaka.

Hadi sasa mwaka 2022 watu 553 wanaripotiwa kuwa wamekufa au hawajulikani walipo na kulingana na miaka iliyopita wengi wamekufa kwenye njia ya kati ya Mediterranean , data zinaonyesha.

XS
SM
MD
LG