Rais wa Utruruki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumanne kwamba watu 35,418 wamekufa nchini mwake, kutokana na tetemeko hilo la 7.8 kwa kipimo cha rikta, na hivyo kulifanya baya zaidi katika historia ya taifa hilo.
Siku 8 baada ya kutokea kwa janga hilo, timu za waokozi zimendelea kutafuta manusura wakati Muhummed Cafer Cetin, mwenye umri wa miaka 18 pamoja na ndugu yake mwenye umri wa miaka 21 wakipatikana wakiwa hai kwenye vifusi vya jengo lao mjini Kahramanamaras, karibu saa 200 tangu lilipotokea.Televisheni za taifa hilo zimeonyesha juhudi za uokozi zikiendelea ingawa wataalam wanasema kwamba matumaini ya kuwapata manusura zaidi yanadidimia kutokana na muda mrefu uliopita.
Wakati huo huo zaidi ya vifo 5,500 vimeripotiwa kwenye nchi jirani ya Syria kulingana na takwimu zilizokusanywa na shirika la kibinadamu la Umoja wa Mataifa, kulingana na ripoti kutoka vyombo vya habari vya ndani. Takriban watu 1,400 wamekufa kwenye eneo linalodhibitiwa na serikali, huku wengine takriban 4,400 wakifa kwenye eneo linalishikiliwa na waasi kaskazini magharibi.
Facebook Forum