Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:43

Idadi ya vifo yaongezeka kutokana na shambulizi la mabomu Uturuki


mtu aliyejeruhiwa akiwa katika gari la kubeba wagonjwa katika uwanja wa ndege wa Ataturk
mtu aliyejeruhiwa akiwa katika gari la kubeba wagonjwa katika uwanja wa ndege wa Ataturk

Mwandishi wa VOA Dorian Jones huko Instanbul amesema mlipuaji mmoja wa mabomu alijilipua nje ya eneo la kupokea wageni wa kimataifa kwenye uwanja huo wa ndege eneo hilo kwa kawaida hujaa watu wakingoja usafiri.

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildrim ametoa wito wa umoja wa kitaifa mapema Jumatano asubuhi ikiwa nchi yake inakumbana na ongezeko la vifo kutokana na shambulizi la kujitoa muhanga liliouwa watu 36 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Atartuk -Instanbul huko Uturuki.

Yildrim akiwa na mawaziri wake amesema idadi hiyo ya waliofariki ni pamoja na walipua mabomu wa kujitoa muhanga watatu ambao waliwasili na gari aina ya taxi Jumanne usiku katika uwanja wa ndege ulio na shughuli nyingi na kufyatua risasi kwa kutumia bunduki rashasha na kupiga risasi watu tofauti waliokuwa uwanjani hapo kabla ya kulipua mabomu wakati polisi wakikaribia.

Mwandishi wa VOA Dorian Jones huko Istanbul amesema mlipuaji mmoja wa mabomu alijilipua nje ya eneo la kupokea wageni wa kimataifa kwenye uwanja huo wa ndege eneo hilo kwa kawaida hujaa watu wakingoja usafiri. Washambuliaji wengine wanaaminika walijaribu kuingia uwanjani hapo ambao unalindwa na polisi wenye silaha nyingi na mashine za X-ray.

Ataturk ni uwanja mkubwa wa ndege wa usafiri wa kimataifa

Ndege zote zilisimamishwa baada ya shambulio hilo lakini waziri mkuu anasema operesheni zimerudi katika hali ya kawaida ilipofika Jumatano asubuhi.

Jumatatu wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitoa onyo kwa wamarekani wanaosafiri kwenda Uturuki.

XS
SM
MD
LG