Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:12

Idadi ya vifo yaongezeka China


Mkoa wa Sichuan uliokumbwa na tetemeko la ardhi, Aprili 20, mwaka 2013
Mkoa wa Sichuan uliokumbwa na tetemeko la ardhi, Aprili 20, mwaka 2013

Zaidi ya watu mia mbili wamefariki kufuatia tetemeko la ardhi Jumamosi na zaidi ya elfu kumi na moja kujeruhiwa katika mkoa wa Sichuan.

Timu za uokozi zinajitahidi kufikia maeneo ya mbali ya mkoa wa Sichuani nchini China ambapo tetemeko kubwa la ardhi limeuwa zaidi ya watu mia mbili na kujeruhi wengine zaidi ya elfu kumi na moja.

Baada ya tetemeko hilo la Jumamosi chombo rasmi cha habari nchini humo kinasema imekuwa vigumu kwa timu za uokozi kufikia maeneo ya Lushuan kupitia barabara na kwamba huduma za simu katika eneo hilo zimekatwa.

Xinhua imesema pia kuwa tetemeko hilo lillitikisa majengo katika mji wa Chengdu, mji mkuu wa mkoa huo wa Sichuan. Yaripotiwa pia kuwa kumetokea mitetemeko mingine midogo katika mkoa huo.

Rais wa China Xi Jinping ameagiza serikali yake kufanya kila juhudi kuokoa walionusurika na kupeleka misaada kwa waathiriwa. Mkasa huo umeibua hisia za machungu kwa wakazi wa Sichuan ambapo watu elfu 70 walifariki kufuatia tetemeko la ardhi mwaka wa 2008.
XS
SM
MD
LG