Zaidi ya vifo 36,000 vimeripotiwa kufikiwa leo, takriban 31, 643 vikitokea Uturuki , huku 4,614 vikiripotiwa Syria. Kwenye mji wa Antakya ambayo kihistoria unajulikana pia kama Antioch nchini Utruruki, hasara iliyopatikana haiwezi kueleleza kwa kuwa kuna majengo yalioporomoka kila mahali. Yale yaliobaki wima yanasemekana kuwa na nyufa, wakati baadhi yakibaki kwenye hali hatari ya kuporomoka.
Serikali imesema kwamba inafanya kila iwezalo, ikizingatiwa kwamba janga hilo limeathiri sehemu yenye ukubwa unaoweza kulinganishwa na Uingereza, na kuathiri takrikban watu milioni 13. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kwamba atajitahidi kukarabati maeneo yalioharibiwa na tetemeko hilo ndani ya mwaka mmoja.
Hata hivyo matumaini ya kupata manusura zaidi yameendelea kudidimia wakati shughuli za uokozi zikikisiwa kusitishwa hivi karibuni. Vikosi vya ulinzi vya Syria ambavyo vinashikilia maeneo yanayoshikiliwa na waasi nchini vimeambia shirika la habari la BBC kwamba shughuli za uokozi zinakaribia kukamilika. Maelfu ya waokoaji wameripotiwa kutafuta manusura usiku kucha nchini Syria na Uturuki.