Wakati idadi ikiongezeka waokoaji waliendelea kufukua vifusi ili kuona kama kuna manusura wowote.
Gavana wa mkoa wa Dnipropetrovsk, Valentyn Reznichenko, amesema kwenye mitandao ya kijamii kuwa shambulio hilo limejeruhi watu 75 na kwamba hali ya wengine 30 haijulikani.
Wafanyakazi wa uokoaji walitumia vifaa kuondoa uchafu siku ya Jumatatu, wakifanya kazi mfululizo kwa matumaini ya kuwapata walio athirika.
Shambulizi hilo la kombora lilifanyika Jumamosi ambapo jeshi la anga ya Ukraine likisema ni kombora la Kh-22 lililorushwa kutoka eneo la Kursk nchini Russia.
Facebook Forum