Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:20

Idadi ya vifo kaskazini mwa Burkina Faso imeongezeka kufikia 86; mamlaka ilisema


Ramani ya Burkina Faso na nchi zilizo jirani nao
Ramani ya Burkina Faso na nchi zilizo jirani nao

Idadi ya vifo kutokana na shambulizi la wikiendi kaskazini mwa Burkina Faso iliongezeka na kufikia saba na kufanya idadi ya waliouawa kufikia 86 mamlaka ilisema Jumatano.

Mauaji hayo katika kijiji cha Seytenga ni ya pili na mabaya sana katika historia ya uasi wa Burkina Faso ambao ulianza mwaka 2015 wakati wanajihadi walipoanzisha mashambulizi ya kuvuka mpaka kutoka Mali.

Mashambulizi hasa ya makundi yenye kushirikiana na al-Qaida na kundi la Islamic State tangu wakati huo yamegharimu maisha ya maelfu ya watu huku karibu watu milioni mbili wakikimbia makazi yao. Idadi ya awali katika shambulizi la Seytenga ilifikia 79.

Wakati huo huo zaidi ya watu 600 kutoka Burkina Faso walikimbilia kaskazini mwa Togo kutafuta usalama kutokana na mashambulizi ya wanajihadi kusini-mashariki mwa Burkina Faso idara ya kitaifa ya ulinzi wa raia Togo iliambia shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG